MAWASILIANO NA DAWATI LA HUDUMA KWA MTEJA LA MAMLAKA YA UDHIBITI WA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo itaendelea kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( COPRA) ili kuboresha zaidi na kulinda mafanikio ya mkoa wa Njombe kwenye uzalishaji na biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko. Mhe. Mtaka ameyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa COPRA Bi.Irene Mlola Ofisini kwake aliyeambatana na kikosi kazi kinachojumuisha wataalamu kutoka COPRA, Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA), Umoja wa Wakulima wa Parachichi (ASTA) kinachofanya kazi ya kubaini changamoto za uzalishaji na biashara ya zao la parachichi katika Wilaya zote zinazozalisha parachichi nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( COPRA), Bi
Irene Mlola leo tarehe 21 Februari, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya. Katika mazungumzo yao, wamejadiliana mikakati ya kusimamia na kuendeleza zao la parachichi katika wilaya yaRungwe mkoni Mbeya. Aidha Mkurugenzi Mlola ameongoza kikao cha Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHP), Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Umoja wa Wakulima wa Parachichi Tanzania (ASTA) na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kujadili namna ya kutatua changamoto zinazolikabiii zao la parachichi.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akiongoza viongozi wa Tanzania kwenye Maonesho ya Pulse Conclave yanayoendelea mjini New Delh nchini India, Februari 2025.
Mhe. Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Hanisa Mbega, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Bi. Irene Mlola, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu, Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano, Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson Ndiege.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko akiongoza viongozi wa Tanzania kwenye Maonesho ya Pulse Conclave yanayoendelea mjini New Delh nchini India, Februari 2025.
Mhe. Dkt. Biteko ameambatana na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Hanisa Mbega, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) Bi. Irene Mlola, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu, Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) Bw. Godfrey Malekano, Mrajisi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dkt. Benson Ndiege.
Mhe. Hassani Iddi Mwamweta, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (ambaye pia anawakilisha Tanzania katika Uswisi, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Romania, Poland, Hungary, Bulgaria, na Vatican), alitembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya kimataifa ya Fruit Logistica mjini Berlin, Ujerumani – 6 Februari 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene M. Mlola, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko kutoka Wizara ya Kilimo, Bi. Happy Kitingati, walifanya ziara ya heshima kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Hassani Iddi Mwamweta. Balozi Mhe. Mwamweta pia anawakilisha Tanzania katika Uswisi, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Romania, Poland, Hungary, Bulgaria, na Vatican. Lengo la kikao hii lilikuwa kuitambulisha rasmi COPRA kwa Ubalozi wa Tanzania na kuangazia mchango wake katika kufungua masoko ya nafaka na mazao mchanganyiko ya Tanzania. Mazungumzo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya COPRA na Ubalozi ili kuongeza mwonekano wa mazao ya Tanzania katika masoko ya Ulaya na kukuza fursa za biashara. Aidha, pande hizo zilijadili njia bora za kuboresha mifumo ya kubadilishana takwimu za biashara za nafaka na mazao mchanganyiko, kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa masoko, kuvutia uwekezaji, na kuimarisha biashara ya mazao ya kilimo katika soko la kimataifa (Februari 2025)
Mkutano huu ulilenga wadau wa sekta binafsi, wakiwemo NGOs, washirika wa maendeleo, na wafadhili, kwa madhumuni ya kushirikiana kuimarisha mifumo ya usalama wa chakula na kuboresha maisha ya wakulima pamoja na wadau wote katika mnyororo wa thamani wa mazao yanayosimamiwa na COPRA. Mkutano wa kwanza wa wadau wa mashauriano kuhusu utekelezaji wa Kanuni za Sheria ya Usalama wa Chakula (Cap. 249) na marekebisho ya Sheria ya Nafaka na Mazao Mengine (Cap. 274) - Desemba 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi amesema yupo tayari kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko COPRA kuhakikisha mifumo ya biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko inafuatwa kama ilivyoelekezwa na serikali. Mhe. Kihongosi ameyasema hayo leo tarehe 7 Januari, 2025 alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko Bi. Irene Mlola alipofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kutambulisha uwepo wa watumishi wa Mamlaka katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwemo Mkoa wa Simiyu. Pichani, katikati Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa COPRA na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao na Viwango kutoka COPRA Bw. Kamwesige Mutembei
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo pamoja na kazi zingine anatambulisha uwepo wa maafisa wa Mamlaka kwa lengo la kuweka mazingira ya utendaji kazi wa pamoja ili kuendesha shughuli za biashara ya nafaka na mazao mchanganyiko yanayolimwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.Picha akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Shigela pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao na Viwango kutoka COPRA Bw. Kamwesige Mutembei - Januari 2025